Deuteronomy 23

Kutengwa Na Mkutano

1 aAsiingie mtu yeyote aliyehasiwa kwa kupondwa makende au kwa kukatwa uume wake katika kusanyiko la Bwana.

2Mtu yeyote ambaye amezaliwa kwenye ndoa isiyo halali au wazao wake wasiingie kwenye kusanyiko la Bwana, hata mpaka kizazi cha kumi.

3 bHapatakuwa na Mwamoni au Mmoabu au yeyote wa wazao wao atakayeruhusiwa kuingia katika kusanyiko la Bwana, hata mpaka kizazi cha kumi. 4 cKwa kuwa hawakuja kuwalaki wakiwa na mkate na maji mlipokuwa njiani mlipotoka Misri, tena walimwajiri Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyoko Aramu-Naharaimu
Yaani Mesopotamia ya Kaskazini-Magharibi.
ili kuwalaani ninyi.
5 eHata hivyo, Bwana Mwenyezi Mungu wenu hakumsikiliza Balaamu bali aligeuza laana kuwa baraka kwenu kwa sababu Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapenda. 6 fMsitafute mapatano ya urafiki nao maisha yenu yote.

7 gUsimchukie Mwedomu, kwa kuwa yeye ni ndugu yako. Usimchukie Mmisri, kwa sababu uliishi kama mgeni katika nchi yake. 8Kizazi cha tatu cha watoto watakaozaliwa nao wanaweza kuingia katika kusanyiko la Bwana.

Unajisi Katika Kambi

9Unapokuwa umepiga kambi dhidi ya adui zako, jitenge na kitu chochote kisicho safi. 10 hIkiwa mtu amechafuka kwa sababu ya kutokwa na shahawa usiku, inampasa atoke nje ya kambi na kukaa huko. 11 iLakini jioni ikikaribia ataoga, na baada ya jua kuzama ataingia tena kambini.

12Tengeni mahali nje ya kambi ambapo mnaweza kwenda kujisaidia. 13Kama sehemu ya vifaa vyenu kuweni na kitu cha kulimia, nanyi mnapojisaidia, chimba shimo na kisha funika kile kikutokacho. 14 jKwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu wenu hutembea katika kambi yenu ili kuwalinda na kuwaweka adui zenu mikononi mwenu. Kambi yenu ni lazima iwe takatifu, ili asione kitu chochote miongoni mwenu kilicho kichafu akageuka na kuwaacha.

Sheria Mbalimbali

15 kIkiwa mtumwa amekimbilia kwako, usimrudishe kwa bwana wake. 16 lMwache aishi miongoni mwenu mahali popote anapopapenda na katika mji wowote anaochagua. Usimwonee.

17 mAsiwepo Mwisraeli mwanamke kahaba au mwanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu. 18 nKamwe usilete mapato ya ukahaba ikiwa ni ya mwanamke au ni ya mwanaume katika nyumba ya Bwana Mwenyezi Mungu wako kwa ajili ya nadhiri yoyote, kwa sababu Bwana Mwenyezi Mungu wako anachukizwa na yote mawili.

19 oUsimtoze ndugu yako riba, iwe ni fedha ama chakula ama kitu kingine chochote ambacho waweza kupata riba juu yake. 20 pUnaweza kumtoza mgeni riba, lakini siyo nduguyo Mwisraeli, ili kwamba Bwana Mwenyezi Mungu wako akubariki katika kila kitu unachoweka mkono katika nchi unayoingia kuimiliki.

21 qUkiweka nadhiri kwa Bwana Mwenyezi Mungu wako, usichelewe kuitimiza, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu wako atakudai, nawe utakuwa na hatia ya dhambi. 22 rLakini ukijizuia kuweka nadhiri, hutakuwa na hatia. 23 sChochote kitakachotamkwa kwa midomo yako ni lazima uhakikishe umekifanya, kwa sababu uliweka nadhiri yako kwa hiari mbele za Bwana Mwenyezi Mungu wako kwa kinywa chako mwenyewe.

24 tKama ukiingia katika shamba la mizabibu la jirani yako, unaweza kula zabibu kadiri utakavyo, lakini usiweke chochote kwenye kikapu chako. 25 uKama ukiingia katika shamba la nafaka la jirani yako, unaweza kukwanyua kwa mikono yako, lakini usikate kwa mundu nafaka iliyosimama.
Copyright information for SwhKC